Isihaka jela miaka 60 kwa kubaka na kulawiti mwanafunzi
Eric Buyanza
February 12, 2026
Share :

Februari 10 ilikuwa ni siku chungu kwa kijana Isihaka Njometi wa miaka 19 mkazi wa Mapinga Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Bagamoyo kumtupa jela miaka 60.
Isihaka amekutana na nyundo nzito toka kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya hiyo Mwamvita Mmanya baada ya kumtia hatiani kwa kosa la Kubaka na Kulawiti.
Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Septemba 28, 2025 mtuhumiwa alimtendea kosa mlalamikaji ambaye jina linahifadhiwa kwa kumbaka na kumlawiti pasipo ridhaa yake msichana wa miaka 13 huku akitambua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Adhabu hii ya kifungo cha miaka 60 inakwenda sambamba kwa makosa yote mawili ambayo kila kosa mtuhumiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 30.
Akizungumza Mahakamani hapo Mrakibu wa Polisi, Hawa Juma ambaye ni kiunganishi baina ya Mahakama, ofisi ya Mashtaka na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, ameipongeza Mahakamani na waendesha mashtaka kutenda haki na wamekuwa wakiwapa ushirikiano mzuri kwenye kesi zinazokuwa zinaendeshwa mahakamani hapo hivyo kuleta matunda ya ushindi.





