pmbet

Israel na Lebanon kuweka silaha chini kwa siku 10

Eric Buyanza

April 17, 2026
Share :

Makubaliano ya siku kumi ya kusitishwa mapigano kati ya Lebanon na Israel yameanza leo Ijumaa (17.04.2026) huku Rais Donald Trump wa Marekani akijaribu kupanga mkutano wa ana kwa ana kati ya pande hizo mbili hasimu.
 

Makubaliano hayo ya kusitishwa mapigano ambayo Trump alikuwa amesema yataanza kutekelezwa saa sita usiku kwa saa za Lebanon na Israel, yanakuja huku Marekani ikiwa inaongeza juhudi za kufikia mkataba wa kusitisha vita na Iran, huku Tehran ikisisitiza kusitishwa vita Lebanon ni lazima kuwe sehemu ya makubaliano yoyote yale.
 

Trump amesema makubaliano ya usitishwaji vita yamekuja kufuatia mawasiliano mazuri ya simu aliyokuwa nayo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Lebanon Joseph Aoun.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet