Israel yaahidi kulipa kisasi kwa shambulio la Golan
Eric Buyanza
July 29, 2024
Share :
Baraza la Usalama wa Taifa la Israel limeipatia idhini serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ya kuamua hatua za kuchukua kujibu shambulizi la roketi lililosababisha vifo vya vijana na watoto 12.
Israel na Marekani zimewalaumu kundi la wanamgambo wa Lebanon la Hezbollah kuhusika na hujuma hiyo ya siku ya Jumamosi lakini kundi hilo limekanusha madai hayo.
DW imeripoti kuwa shambulio hilo kwenye kitongoji cha Majdal Shams ndilo baya zaidi kutokea ndani ya Israel au katika maeneo inayoyakalia tangu uvamizi wa kundi la Hamas wa Oktoba 7 mwaka jana, uliosababisha kuzuka kwa vita vya Gaza.
Israel iliapa kwamba itajibu shambulizi hilo dhidi ya Hezbollah na tayari jana Jumapili ndege za kivita za nchi hiyo ziliyapiga maeneo kadhaa ndani ya Lebanon.