Israel yadai kulipa kisasi, kwa kumuua Kamanda ya Hezbollah ndani ya Lebanon
Eric Buyanza
July 31, 2024
Share :
Jeshi la Israel jana Jumanne jioni lilisema lilifanya shambulio mjini Beirut likimlenga kamanda wa Hezbollah, Fuad Shukr, ambaye linadai alihusika na shambulio la anga ambalo liliua watoto 12 na vijana waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wa mpira mwishoni mwa wiki iliyoisha katika milima ya Golan.
Mlipuko mkubwa ulisikika, na moshi mwingi ulionekana ukitanda juu ya vitongoji vya kusini mwa Beirut, ngome ya wanamgambo wa Hezbollah wanaofadhiliwa na Iran.
Afisa wa Hezbollah alisema majengo kadhaa yaliharibiwa na mamlaka ilisema watu wawili waliuawa.
Chombo cha habari cha Saudia Al Hadath kiliripoti kwamba Shukr alinusurika. Lakini tovuti ya habari ya Israel Ynet ilikinukuu chanzo cha usalama cha Israel kikisema.
“Kuna uwezekano mkubwa afisa huyo wa Hezbollah aliuawa. kama alikuwa katika jengo hilo, hayuko nasi tena.”
VOA