pmbet

Israel yapiga marufuku magari ya kichina kwa sababu za kiusalama

Eric Buyanza

June 15, 2026
Share :

Israel imeamua kuachana na magari ya umeme ya China kwa ajili ya jeshi lake.

Hii imekuja wiki moja tu baada ya Marekani kuchapisha orodha ya makampuni ya Kichina yaliyopigwa marufuku kuuza magari kwa jeshi la Marekani kutokana na madai ya kampuni hizo kuhusishwa na jeshi la China.
 

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Haaretz, uliochapishwa siku ya Jumapili, Juni 14, unaonyesha kwamba jeshi, pamoja na idara za ujasusi za Israel na hata makampuni kadhaa ya ulinzi, yamepunguza kwa wingi matumizi ya magari ya umeme ya China.
 

Makampuni ya China yanayotengeneza magari hayo yanachangia karibu nusu ya mauzo ya magari nchini Israel.
 

Serikali ya Israel ina wasiwasi na hofu kwamba data nyeti zilizokusanywa na magari haya zinaweza kuishia mikononi mwa jeshi la China.
 

Hata hivyo, kampuni ya BYD inayoongoza kwa kutengeneza magari nchini China, imekana kuhusishwa na jeshi la China.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet