pmbet

Israel yashambulia kambi mbili za ulinzi wa anga za Syria

Eric Buyanza

July 30, 2024
Share :

Shirika linalofuatilia masuala ya haki za binadamu la Syria limesema mashambulizi ya Israel yamezipiga kambi za ulinzi kusini mwa Syria usiku wa kuamkia leo. 

Hayo yanatokea wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka katika mpaka wa kaskazini wa Israel kufuatia shambulizi lililosababisha vifo katika milima ya Golan. 

Shirika hilo halikuripoti maafa wala majeruhi yoyote katika mashambulizi hayo ya usiku kucha katika mkoa wa Daraa, ulioko katika eneo linalovitenganisha vikosi vya Syria na Israel katika milima ya Golan. 

Chombo cha habari ya serikali ya Syria hakikuripoti mashambulizi yoyote. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Naetanyahu ameapa kuchukua hatua kali kujibu shambulizi la Jumamosi iliyopita lililowaua vijana 12 katika mji wa jamii ya kiarabu ya Druze katika milima ya Golan. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet