pmbet

Israel yashambulia shule ya (UN) Gaza na kuua wapalestina 32

Eric Buyanza

June 6, 2024
Share :

Vikosi vya Israel vimeshambulia kwa bomu shule yenye uhusiano na Umoja wa Mataifa katikati mwa Gaza na kuua takriban Wapalestina 32 waliokimbia makazi yao na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Hamas, ambayo inayotawala Ukanda wa Gaza, imelaani shambulio hilo na kuliita la "Mauaji ya kutisha" na kusema wanawake na watoto wengi walikuwa miongoni mwa waliouawa na kujeruhiwa.

Shirika la habari la Palestina (Wafa) limethibitisha idadi ya waliofariki kuwa ni 32.

Shirika hilo limesema kuwa maelfu ya Wapalestina waliokimbia makazi yao walikuwa wakijihifadhi katika shule hiyo iliyoko kwenye kambi ya Nuseirat ya al-Sardi, ambayo inahusishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA.
AL JAZEERA

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet