pmbet

Israel yashambuliana na Hezbollah nchini Lebanon

Eric Buyanza

April 9, 2026
Share :

Ni zaidi ya saa 24 tangu Rais wa Marekani Donald Trump atangaze kusitisha mapigano kwa wiki mbili nchini Iran, jambo ambalo Israel, Iran na wapatanishi wa Pakistan walilithibitisha.
 

Lakini tayari makubaliano ya amani yanaonyesha kuyumba.

Israel imeanzisha wimbi kubwa la mashambulizi nchini Lebanon, na kuua watu wasiopungua 182.
 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea mashambulizi hayo kama "pigo kubwa zaidi" kwa Hezbollah tangu kuanza kwa vita, akisema Israel itaanza tena kupigana na Iran kukiwa na haja ya "kufanya hivyo".

 

Wakati huo huo, Iran imesema ikiwa mashambulizi nchini Lebanon hayatakoma mara moja huenda yakachochea "hatua kuchukuliwa".
 

Siku ya Jumamosi, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance atashiriki katika mazungumzo na Iran mjini Islamabad, Pakistan.

 

Jambo la msingi litakuwa usafiri wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz, njia ya baharini katika Ghuba ya Uajemi ambayo ni muhimu kwa usambazaji wa mafuta duniani.

Iran imesema meli "zitalengwa na kuharibiwa" ikiwa zitapita bila ruhusa.

Spika wa bunge la Iran pia anasema mambo matatu ya kusitisha mapigano kwenye mapendekezo yenye masuala 10 "yamekiukwa waziwazi", huku Vance akisema kila mara kuna "mapungufu" katika makubaliano kama hayo.

 

HEZBOLLAH YASEMA IMESHAMBULIA KASKAZINI MWA ISRAEL

Vile vile, Hezbollah imesema imerusha makombora kaskazini mwa Israeli.
 

Wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran wanasema ilikuwa ni kujibu ukiukwaji wa mapigano, katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
 

Pia wametishia kuendelea na mashambulizi hadi "uchokozi wa Israel na Marekani" dhidi ya Lebanon utakapokoma.
 

Bado kuna kutokubaliana kuhusu kama nchi hiyo imejumuishwa katika usitishaji mapigano.

 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet