Israel yaua watoto watatu wa kiongozi mkuu wa Hamas
Eric Buyanza
April 11, 2024
Share :
Israel Jumatano iliwaua watoto watatu wa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh katika shambulio la anga huko Gaza, ikisema ndugu hao walikuwa wanachama wa tawi la kijeshi la Hamas.
Wajukuu wanne wa Haniyeh waliuawa pia katika shambulio hilo.
Haniyeh amethibitisha vifo hivyo katika mahojiano na kituo cha matangazo cha Al Jazeera, akisema watoto wake “waliuawa kama mashujaa kwenye barabara wakijielekeza kukomboa Jerusalem na msikiti wa Al-Aqsa.
“Adui mhalifu anaongozwa na roho ya kulipiza kisasi na mauaji na hathamini vigezo au sheria zozote,” Haniyeh alisema.
Watoto wake ni miongoni mwa maafisa wakuu kuuawa katika vita vya miezi sita kati ya Israel na Hamas huko Gaza.
Jeshi la Israel limewataja ndugu hao watatu, mmoja kama kamanda na wawili kama maafisa wa kijeshi.