pmbet

Israeli yajibu mashambulio ya Iran

Eric Buyanza

June 8, 2026
Share :

Jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi magharibi na katikati mwa Iran alfajiri ya leo ikiwa ni saa kadhaa tangu Tehran ilipovurumisha makombora kuelekea Israel.

 

Taarifa ya jeshi hilo imesema kwa maelekezo ya Idara ya Ujasusi ya Jeshi, ndege zake za kivita zimeyalemga maeneo kadhaa ya Iran na kwamba taarifa ya kina itatolewa baadaye. Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti milipuko kwenye mji mkuu Tehran na mijinge ya Tabriz, Isfahan na Karaj.

 

Mapema jana usiku, Iran ilifyetua mkururo wa makombora ya masafa pamoja na droni kuilenga Israel, katika shambulizi lake la kwanza tangu kufikiwa makubaliano legelege ya kusimamisha vita kwa muda mnamo mwezi Aprili.

 

Ving´ora vya tahadhari vililia kwenye maeneo kadhaa ndani ya Israel na kuwalazimisha milioni ya raia wa taifa hilo kukimbilia kwenye mahandaki. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet