Israeli yasema vitisho vya Iran havitaizuia kujibu mashambulizi
Eric Buyanza
April 17, 2024
Share :
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant amesema vitisho vya Iran havitazuia taifa lake kujibu mashambulizi ya anga ya Jumapili dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.
Katika ziara yake kaskazini mwa Israel, Wizara ya huyo alinukuliwa akisema, "Wairani walishindwa katika shambulio lao na watashindwa kuizuia Israel kutekeleza mpango wake."
Maafisa wa Iran walitoa onyo kwa Israel kwamba isithubutu kulipiza, na kuapa kwamba kama italipiza basi Tehran itajibu kwa kishindo.