"Itakuwa mwisho wenu” beki wa Czech awatisha Bafana Bafana
Eric Buyanza
June 17, 2026
Share :
Beki wa Jamhuri ya Czech, Jaroslav Zelený amekichimba mkwara kikosi cha timu ya Taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) kuwa Alhamisi itakuwa mwisho wao watakapokutana kwenye mchezo wao jijini Atlanta
Wakiwa wamepoteza mechi yao ya ufunguzi ya Kombe la Dunia kwa mabao 2-1 dhidi ya Korea Kusini, Czech wana matumaini kuibuka na ushindi dhidi ya Afrika Kusini.
Zelený anaamini timu yake iko vizuri kuliko Bafana na anatarajia mchezo wa nguvu huku timu zote zikitafuta ushindi wao wa kwanza wa michuano hiyo.






