Ivan Rakitic atangaza rasmi kustaafu soka.
Joyce Shedrack
July 7, 2025
Share :
Nyota wa zamani wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Croatia Ivan Rakitić amestaafu rasmi kucheza soka akiwa na umri wa miaka 37 baada ya kucheza jumla ya mechi 971 na kushinda mataji 17.
Rakitić alifanikiwa kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja na mataji manne ya Uhispania akiwa na Barcelona huku akishinda UEFA Europa League akiwa na Sevilla pia alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Dunia 2018 mbele ya bingwa Ufaransa.