Ivan Toney anasubiria mwenye kisu kikali kati yao
Eric Buyanza
April 11, 2024
Share :
Klabu za Arsenal na Chelsea za nchini Uingereza zinamfuatilia kwa karibu sana mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Uingereza, Ivan Toney.
Toney mwenye umri wa miaka 28 kwasasa yuko chini ya mkataba hadi 2025, na dau la kumnyakua kwasasa inaelezwa kuwa limeshuka kutoka pauni milioni 100 zilizokuwa zikisemwa hapo awali hadi kufikia pauni milioni 60 mpaka 40.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao 20 ya Ligi Kuu msimu uliopita, na kuzidiwa na Harry Kane pamoja na Erling Haaland.
Alihusishwa sana na kuondoka Januari, lakini hakuna kilichotokea labda kutokana na dau kubwa ambalo klabu yake Brentford walikuwa wakitaka.