Ivan Toney hatadumu kwa muda mrefu Arsenal - Rio Ferdinand
Eric Buyanza
February 13, 2024
Share :
Gwiji wa Manchester United, Rio Ferdinand amedai mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney "hatadumu kwa muda mrefu" Arsenal ikiwa atajiunga na klabu hiyo kwenye majira ya joto.
Toney alihusishwa na The Gunners kwenye dirisha la Januari, lakini The Bees walitaka pauni milioni 100 kwa mchezaji huo.
Arsenal wanatarajiwa kurejea mwishoni mwa msimu huu kwa mchezaji huyo, huku kocha wa Brentford, Thomas Frank akikiri kwamba Toney huenda akaondoka.