Jacob Zuma anusurika kwenye ajali, gari lake likigongwa na mlevi
Eric Buyanza
March 29, 2024
Share :
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amenusurika katika ajali ya gari baada ya gari lake kugongwa na dereva aliyekuwa amelewa, polisi wamesema.
Dereva mwenye umri wa miaka 51 amekamatwa akishtakiwa kuendesha gari akiwa amelewa, ilisema taarifa ya polisi iliyotolewa mapema leo Ijumaa.
Zuma na walinzi wake walichomoka bila kujeruhiwa.
Msemaji wa chama cha MK Nhlamulo Ndhlela alidai kuwa ajali hiyo ya gari haikuwa ya bahati mbaya na ililengwa mahsusi katika msafara huo.
Chama cha uMkhonto weSizwe (MK) ndicho ambacho Jacob Zuma anakipigia kampeni kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Mei.