Jake Paul kuzichapa na Francis Ngannou hivi karibuni
Sisti Herman
March 27, 2026
Share :

Mwanamitandao maarufu Jake Paul aliyetoka kupigana hivi karibuni na kuvunjwa taya na Antony Joshua, anahusishwa kutaka pambano dhidi ya bingwa wa zamani wa UFC, Francis Ngannou.
Ngannou anajulikana kwa nguvu zake za ajabu za kupiga (knockout power), jambo ambalo lingekuwa mtihani mzito zaidi kwa Paul kama ilivyokuwa dhidi ya A.J mwishoni mwa mwaka uliopita.
Pambano hili linatazamwa kama tukio ambalo linaweza kuingiza fedha nyingi na kuvuta hisia za mashabiki wa MMA na Boxing duniani kote.





