Jamaa alazimisha talaka, baada ya kuota ndoto mke wake anamsaliti
Eric Buyanza
July 15, 2024
Share :
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja kutoka Bulawayo nchini Zimbabwe aliyefahamika kwa jina la Energy Moyo ameiomba Mahakama ya Kimila ya Bulawayo imuachanishe na mkewe (talaka) baada ya kuwa anapata ndoto za mara kwa mara zikimuonyesha kuwa mke wake anamsaliti na mwanaume mwingine.
Energy Mkazi wa kitongoji cha Lobenvale, alimuoa Angela Dube miaka tisa iliyopita na sasa anataka waachane akitaja ndoto anazoota zinamuonyesha wazi kabisa kuwa mke wake sio mwaminifu.
Zaidi ya hayo, Moyo alidai kuwa kila anapojaribu kutaka kujadili ndoto hizo na mwenzake, amekuwa akipokea matusi mazito kutoka kwa mkewe.