pmbet

Jamaa apika na kula kidole chake mwenyewe

Eric Buyanza

June 16, 2026
Share :

Mwaka 2013 huko kwenye jiji la Colchester nchini Uingereza kidole na sehemu ya mkono wa David Playpenz viliharibika vibaya kutokana na ajali ya pikipiki,  lakini baada ya madaktari kupendekeza viungo hivyo vikatwe kutokana na kuharibika....David aliomba kuondoka navyo nyumbani....na kilichotokea huko anayejua ni mola.


ILIKUAJE?

Baada ya madaktari kumaliza upasuaji wa kuondoa viungo hivyo,  David kutoka aliwauliza madaktari ikiwa angeweza kuondoka na kidole chake kilichoharibika na kukatwa na hawakuwa na pingamizi lolote.

 

David anasema siku zote alikuwa akitamani kujua utamu wa nyama ya binadamu lakini hakujua mahali pa kuipata, hata hivyo baada ya kugundua kuwa hakuna mtu anayeweza kumburuza mahakamani kwa kula nyama yake mwenyewe, aliamua kukipika chukuchuku bila chumvi kidole hicho na kukitafuna.

 

Kwa mujibu wa jamaa huyu ambaye wengi walihisi ameshikwa na wazimu, kupoteza kidole kwake lilikuwa jambo kubwa lililomhuzunisha sana na hivyo yeye kuamua kula kidole chake ni kama kujipa faraja kwamba hajapoteza sehemu yake ya mwili wake.

Dunia ina mambo!

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet