Jamaa hulipwa milioni 52, kila akipanda mnara huu kubadilisha Balbu
Eric Buyanza
May 30, 2024
Share :
Kupanda mnara wa mawasiliano wa futi 1,500 kunaweza kuonekana kama kazi isiyowezekana kwa wengi wetu, lakini kwa Kevin Schmidt, ni kazi ya kawaida sana kwake.
Schmidt hupanda mnara huu kila baada ya miezi sita ili kubadilisha balbu.
Kazi hii ya kutisha na ya kipekee inayo ogopwa na wengi humuingizia Kevin Dollar 20,000 (sawa na milioni 52 za kibongo) kila anapopanda.
Mnara huu kule juu kabisa kileleni una taa nyekundu kwa ajili kuzionya ndege ili zisipite karibu na mnara huo.