Jambazi wa zamani aukwaa Uwaziri wa Michezo Afrika Kusini
Eric Buyanza
July 3, 2024
Share :
Gayton McKenzie, mwanasiasa wa upinzani ambaye safari yake ya maisha ilizungukwa na matukio kadha wa kadha kuanzia kuwa jambazi sugu hadi mmiliki wa klabu ya burudani yenye utata, sasa ameteuliwa kuwa waziri wa michezo, sanaa na utamaduni wa Afrika Kusini.
Rais Cyril Rampahosa alimteua Bw McKenzie - Kiongozi wa Muungano wa Patriotic (PA) - kwenye wadhifa katika serikali ya vyama vingi ambayo aliitangaza Jumapili baada ya chama chake cha African National Congress (ANC) kupoteza wingi wake wa wabunge katika uchaguzi wa Mei 29.
Uteuzi wa Bw McKenzie wake ni ishara ya jinsi alivyoshinda dhiki ili kupata mafanikio.
Aliiba benki mara ya kwanza kabla ya kufikisha umri wa miaka 16, kisha akawa jambazi kamili. Alisema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha redio, alikaa gerezani kwa miaka saba, na akaapa kubadilika baada ya kuachiliwa.
"Ningeweza kuwa na randi 12 mfukoni mwangu lakini nilikuwa na randi bilioni moja akilini mwangu. Na hilo ndilo watu hawaelewi - wanazingatia kile wanachokosa badala ya jinsi ya kupata kile wanachokosa," alisema katika mahojiano ya 2013 na shirika la utangazaji la SABC.
BBC