pmbet

"Jambo la Damaro na sisi tupo nalo Serious"Magori.

Joyce Shedrack

April 7, 2026
Share :

Mwenyekiti wa Bodi wa Simba Crescentius Magori Amesema wapo serious na kesi ya kiungo wa Yanga Mohamed Damaro kuhusu Uraia wa mchezaji huyo.

 

“Hili jambo sio fair sababu kuna timu moja ina wachezaji 13 kwa kutumia mlango wa nyuma. Na aliyedanganya mamlaka kwamba anapewa uraia ili acheze timu ya taifa basi alifanya udanganyifu mkubwa, unampa uraia wa nini tena mchezaji mwenyewe hana hata mwaka Tanzania. Ni jambo serious na sisi tupo nalo serious.”

“Mashabiki wetu wametaharuki, wamekuwa na hasira, nafahamu mashabiki wetu wanakerwa na hili jambo na wanaona yanayotokea lakini niwasihi sana watulie. Sisi Simba ni timu ambayo inaweka mpira wa miguu mbele, najua mpira una hasira kubwa. Bodi tunalishughulikia na tumeiandikia mamlaka, tutakutana nao na watatuambia kwanini hayo mamabo yanatokea mara kwa mara.”- Mwenyekiti wa Bodi wa Simba Crescentius Magori.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet