pmbet

Janga la ajira ni bomu linasubiri kulipuka - Ado Shaibu

Eric Buyanza

July 26, 2024
Share :

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amesema Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe kuwa mipango ya uwezeshaji wa wakulima inapaswa kujikita vijijini ili kuwawezesha wakulima halisi na kuongeza tija katika uzalishaji.

Amesema kuna mradi huu wa BBT. Fikra ya kuwawezesha wakulima ni fikra njema,lakini, mpango ulipaswa kujikita vijijini. H”uko ndiko waliko Wakulima halisi,mtindo wa wizara kukusanya vijana mijini, kuwapa mikopo, ardhi na nyenzo, hautaleta matokeo makubwa na mpango utafeli kama ilivyofeli mipango iliyotangulia ya kilimo”,amesisitiza .

“Janga la ajira ni bomu linasubiri kulipuka. Ili kukabiliana nalo, pamoja na mambo mengine ni lazima tuboreshe kilimo na shughuli nyingine za uzalishaji vijijini kwa kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za uhakika, bei nzuri za mazao na mikopo yenye riba nafuu kuongeza tija katika kilimo na ufugaji”amesema Ado. 
TM

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet