Januari ni mwezi wangu wa majaribio, mwaka mpya wangu unaanza Februari
Eric Buyanza
January 25, 2024
Share :
Nyota wa muziki wa Nigeria, mwanadada Tiwa Savage amesema kuwa mwaka wake wa 2024 utaanza siku ya Februari 1.2024.
Tiwa alibainisha hayo alipoutangaza mwezi Januari kama mwezi wake wa majaribio.
KUpitia ukurasa wake wa Instagram aliandika.... "Nimeamua kwamba 2024 yangu itaanza Februari 1, Januari bila shaka ni mwezi wa majaribio.”