Jaribio la kutoroka jela lilivyogeuka kichekesho kikubwa
Eric Buyanza
March 21, 2026
Share :
#JeWajua Huko nchini Brazil, mfungwa mmoja alitumia miaka mitano kuchimba handaki la siri chini kwa chini ili aweze kutoroka jela.
Baada ya muda mrefu wa kuandaa mpango huo huku akiweka juhudi katika kazi hiyo kwa usiri mkubwa, hatimae juhudi zake ziligeuka kuwa kichekesho kikubwa kwani pale alipopanga aende kuibukia kilikuwa ni chumba cha askari wa gereza hilo.






