pmbet

Jay Z kusimamia wachezaji wa Africa

Sisti Herman

July 23, 2025
Share :

 

Kampuni ya usimamizi na uwakala wa michezo Roc Nation Sports ya msanii wa Hip Hop Jay-Z inahamia katika soko la soka barani Afrika ili kuvumbua na kuendeleza vipaji vya vijana.

Kampuni hiyo ya uwakala imesajili wachezaji nane kutoka nchi za Afrika Kusini, Nigeria, na Ghana, ikiwa ni pamoja na majina maarufu kama Siyabonga Mabena na Ifeoluwa Olowoporoku.

Pia kampuni hiyo ambayo inasimamia nyota kama Vinícius Jr na Reece James, linalenga kusaidia wachezaji wa Kiafrika ndani na nje ya uwanja.

RNSI pia inapanga kujitanua hadi Ivory Coast, Tanzania na Zambia, na kufungua milango zaidi kwa fursa za soka duniani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet