Jayrutty kuwakabidhi nyota wa kigeni wa Simba magari.
Joyce Shedrack
March 5, 2026
Share :
Kiungo mshambuliaji wa klabu a Simba Inno Jospin Loemba amekabidhiwa Gari aina ya CROWN New Model na Kampuni ya JAYRUTTY Investment kupitia Mkurugenzi wake CPA Joseph Rwegasira ambaye ndio mzabuni wa jezi na vifaa vyote vya Simba.
Loemba ni mchezaji wa Simba aliyesajiliwa na Kampuni ya JAYRUTTY kama ambavyo mkataba wake na Simba ulisema kuwa atasaidia kusajili mchezaji mmoja kila msimu.
Kampuni hiyo pia itatoa magari kwa Libasse Gueye, Anicet Oura na Djibrilla Kassali, kama baadhi ya makubaliano ya kimkataba mkataba wake yanavyosema.





