Jd Vance aionya Iran kutofanya mzaha na Marekani
Eric Buyanza
April 11, 2026
Share :

Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance ameelekea Islamabad nchini Pakistan ambapo atashiriki mazungumzo ya amani na Iran yenye lengo la kuyaokoa makubaliano ya usitishwaji mapigano kwa muda wa wiki mbili ambayo yako hatarini kuvunjika.
Vance ameionya Iran "kutofanya mzaha" na Marekani lakini akasema anataraji kuwa mazungumzo ya Islamabad yatakuwa chanya na huenda yakapunguza hali iliyopo ya mvutano hasa kuhusu vipengele vya makubaliano hayo.
Rais Donald Trump amewapa jukumu la kusimamia mazungumzo hayo maafisa wake wa karibu akiwemo JD Vance , ambao walionekana wazi kupinga operesheni hiyo ya kijeshi nchini Iran. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kujadili miongoni mwa mambo mengine, mpango wa nyuklia wa Iran na kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
DW





