Je unajua kuwa maji ya bahari yana dhahabu?
Eric Buyanza
July 23, 2026
Share :
Ndio ni kweli, wanasayansi wamethibitisha kuwa maji yote ya bahari duniani yana madini ya dhahabu ndani yake.
Hata hivyo, dhahabu hiyo imesambaa kwa kiwango kidogo mno kiasi kwamba huwezi kuiona kwa macho. Kwa wastani, utapata gramu moja tu ya dhahabu katika kila tani milioni 100 za maji ya bahari.
Gharama ya nishati, mitambo na kemikali zinazohitajika kuchuja mamilioni ya lita za maji ili kupata kiasi kidogo cha dhahabu ni kubwa kuliko thamani ya dhahabu yenyewe. Ndio maana hadi sasa hakuna nchi au kampuni inayochimba dhahabu kutoka kwenye maji ya bahari.






