JE, WAJUA: Aliibwa Afrika ili akaonyeshwe kwenye maonyesho ya wanyama
Eric Buyanza
April 11, 2024
Share :
Ota Benga, mtoto aliyenunuliwa na mfanyabiashara wa kimarekani Samuel Philips Verner kutoka nchini Congo mwaka 1904 na kupelekwa Marekani.
Mnamo September 1906, aliwekwa kwa siku 20 kwenye bustani ya maonyesho ya wanyama mjini Bronx (Bronx Zoo) na kuwa kivutio kikubwa kwa watu weupe waliokuja mara kwa mara kumtazama kama kivutio.
Watoto kwa watu wazima walifika sio kumshangaa tu, bali kumcheka na kumdhihaki kwa kumrushia ndizi kama vile inavyokuwa kwa nyani au tumbili.
Ghadhabu kutoka kwa mawaziri wa Kikristo ilitamatisha kushikiliwa kwake na alihamishwa hadi hifadhi ya yatima weusi ya Howard New York iliyokuwa inasimamiwa na mchungaji Mmarekani Mweusi James H Gordon.
Januari 1910 alipelekwa kwenye seminari ya kitheolojia kwa wanafunzi weusi huko Virginia.
Baadae inaelezwa alipata ugonjwa wa sonona (stress) kutokana na kutamani kurudi nyumbani kwao na Machi 1916 akajipiga risasi kwa bunduki ambayo alikuwa ameificha. Inakadiriwa kwamba wakati huo alikuwa na umri wa karibia miaka 25.