JE, WAJUA: Asababisha mafuriko makubwa, ili aweze kustarehe na mchepuko
Eric Buyanza
March 9, 2024
Share :
Mwaka 1993, James Scott wa Missouri nchini Marekani alifanya tukio ambalo mpaka leo hii limeendelea kushangaza watu kote duniani.
ALIFANYAJE?
Bwana James aliamua kuharibu kingo za mto Missisipi kwa nia ya kusababisha mafuriko.
ILI IWEJE?
Alifanya hivyo ili kumchelewesha mke wake asirudi nyumbani mapema ili apate kuburudika na kufurahia maisha na mchepuko wake.
NINI KILITOKEA
James alisababisha mafuriko makubwa kuwahi kutokea yaliyodumu kwa miezi 4, na alihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa hilo.