JE WAJUA: Asili ya neno KILIMANJARO ni KILIMAKYARO
Eric Buyanza
July 4, 2024
Share :
Neno KILIMANJARO ni makosa ya kimatamshi yaliyofanywa na wageni (wakoloni enzi hizo).
Wazawa wenyewe (wachaga) walikuwa wakiuita Mlima huo kwa lugha yao KILIMA KYARO wakimaanisha (Kilima kirefu) lakini makosa ya kimatamshi ya wageni kushindwa kulitamka neno hilo la kichaga ndiyo chanzo cha kuzaliwa neno Kilimanjaro.
Kwa hiyo KILIMAKYARO ndio jina halisi lakini kwasasa tunaufahamu kama KILIMANJARO.