JE, WAJUA: Bob marley alipewa nishani ya amani na Umoja wa Mataifa?
Eric Buyanza
March 26, 2024
Share :
Bob Marley atakumbukwa sana kwa nyimbo zake za kijamii na kisiasa, Lakini je, unajua kwamba mwaka 1978 mwanamuziki huyu wa muziki wa Reggae alitunukiwa nishani ya amani na Umoja wa Mataifa?
Tuzo hiyo aliyopewa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya mwanamuziki huyo katika kukuza amani na haki wakati wa machafuko ya kisiasa nchini Jamaica.
Mapema mwaka 1978, Marley alitumbuiza katika Tamasha la Amani la ‘One Love' huko Kingston, Jamaica.
Tamasha hilo lililenga kupunguza ghasia za magenge ya kidini na Marley alikuwa amewaleta pamoja wapinzani wa kisiasa kupeana mikono jukwaani.
Tuzo hiyo ya Umoja wa Mataifa ilitolewa miezi michache baada ya Tamasha hilo katika ukumbi wa Waldorf Astoria mjini New York nchini Marekani, na iliwasilishwa na wajumbe wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa.