JE, WAJUA: George alitengwa kwa kuwa mweusi, akawaburuza kwa ufaulu
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
McLaurin alikuwa mwanamume wa kwanza mweusi kusoma katika Chuo Kikuu cha Oklahoma nchini Marekani mnamo mwaka 1948.
Akiwa chuoni hapo alitengwa na kulazimishwa kuketi peke yake kwenye kona ya darasa mbali kabisa na wanafunxi wenzake kwa kuwa alikuwa mtu mweusi pekee chuoni hapo.
Hata hivyo jina lake limebakia kwenye orodha ya heshima kama mmoja wa wanafunzi watatu bora chuoni hapo.
Hii ilitokana na matokeo yake Bora ya kitaaluma.