JE WAJUA: Kabla ya kuwa mwanamuziki Bob Marley alikuwa mtabiri
Eric Buyanza
February 13, 2024
Share :
Kabla ya kuwa mwanamuziki, Bob Marley alikuwa msomaji viganja katika mji aliozaliwa wa St Ann huko Jamaica.
Akiwa mtoto, alisoma viganja vya marafiki na majirani ili kuwaambia yale yatakayotokea wakati ujao.
Kulingana na rafiki wa karibu wa mwimbaji huyo, Allan "Skill" Cole, utabiri mwingi wa Marley ulikuwa na kiwango cha usahihi.
Lakini Cole, ambaye alisimamia ziara za matamasha ya Marley katika miaka ya 1970, anasema utabiri wa kusoma viganja ulipingwa sana nchini Jamaica wakati huo.
Jumuia ya Rastafary iliyokuwa karibu na Bob Marley, ilimshawishi kuacha kusoma viganja...jambo ambalo alikubali.