pmbet

JE WAJUA: Kijana aliingia mtaani na Simba ili kupambana na mbwa wa polisi

Eric Buyanza

March 23, 2024
Share :

Mwaka 2019 huko nchini Iraq kulipokuwa na ripoti kwamba vikosi vya usalama vya Iraq vingetumia mbwa kuzuia waandamanaji kuingia barabarani, kijana mmoja wa kiiraki aliamua kuchukua hatua za kibabe kwa kuingia barabarani na simba wake kipenzi.
 

Nia ya kijana huyo ilikuwa kumuachilia mnyama huyo mkali ili kuwatawanya mbwa wa polisi waliokusudiwa kuwadhibiti waandamanaji.
 

Hata hivyo polisi wala mbwa wao hawakuonekana eneo la tukio na maandamano hayo yaliendelea kama yalivyopangwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet