JE, WAJUA: Mamba anaweza kulala jicho moja likiwa wazi?
Eric Buyanza
February 23, 2024
Share :
JE, WAJUA
Wataalamu wa masuala ya wanyama wanasema kwamba, mamba ana uwezo wa kulala usingizi kabisa huku jicho lake moja likiwa wazi.
HII INAKUAJE?
Utafiti uliOfanyika umeoyesha kuwa hali hiyo ya kulala jicho moja likiwa wazi hutokea kwa sababu sehemu moja ya ubongo wa mamba huwa imezima, wakati sehemu nyingine ikiwa inafanya kazi.
Kwa mfano wanasayansi wamebainisha kwamba kusinzia kwa jicho moja ni jambo la kawaida kwa baadhi ya ndege, kama vile pomboo ambao huendelea kuangalia kwa nusu ya ubongo wao, wakati nusu nyingine ya ubongo ikiwa imepumzika.