pmbet

JE, WAJUA: Mashine ya kwanza ya ATM ilifungwa jijini London 27 June 1967

Eric Buyanza

May 11, 2024
Share :

Mashine ya kwanza ya ATM ilifungwa kwenye tawi la Bank ya Barclays huko Enfield, Kaskazini mwa jiji la London tarehe 27 June mwaka 1967.

Wakati mvumbuzi wa mashine hizo, John Shepherd Baron alipounda mashine hizo kwa mara ya kwanza, zilikuwa zinatumia neno la siri/Password yenye tarakimu 6.

Hata hivyo haikuchukua muda Bwana John alibadilisha na kuifanya itumie password ya tarakimu 4 baada ya kuambiwa na mkewe.

Bwana John anasema mke wake alimwambia hawezi kukariri tarakimu zaidi ya 4.

John alizaliwa India mwaka 1925 na kufariki mwaka 2010 huko Scotland akiwa na umri wa miaka 84.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet