Je wajua? Mchezaji ghali zaidi wa kike duniani ni Mzambia
Sisti Herman
February 14, 2024
Share :
Mshambuliaji wa timu ya Taifa wanawake ya Zambia Racheal Kundananji ameandika rekodi kuwa mchezaji ghali zaidi wa kike duniani mara baada ya uhamisho wake kutoka Madrid CFF ya ligi kuu wanawake nchi Hispania kwenda US club Bay FC ya ligi kuu wanawake nchini Marekani kugharimu dola za kimarekani 787,800 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 2 za Titanzania
Mshambuliaji huyo wa Copper Queens (jina la utani la timu ya Taifa Zambia) alimaliza nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu wananwake nchini Hispania msimu jana akiwa na magoli 25.