pmbet

JE WAJUA: Mechi ndefu zaidi ya soka duniani, yaisha baada ya masaa 26

Eric Buyanza

June 20, 2024
Share :

Mwezi ulioisha kwenye Uwanja wa Olimpiki wa Luzhniki ulioko nje kidogo ya jiji la Moscow huko nchini Urusi, uliandaliwa mchezo mrefu zaidi wa kandanda kuwahi kutokea duniani uliokisha baada ya masaa 26. 

Timu mbili za wachezaji 7 kila moja zilikusanyika kwenye Uwanja huo kuvunja rekodi ya mechi ndefu zaidi ya kandanda kuwahi kutokea. Mchezo huo ulianza Jumamosi mchana na kumalizika kesho yake Jumapili saa 8 mchana. 

Rekodi ya awali iliwekwa mwaka 2014 wakati timu mbili zilipocheza kwa masaa 24 mfululizo. 

Mpaka mwisho wa mchezo timu iliyoshinda ilikuwa na jumla ya mabao 416 dhidi ya mpinzani wake aliyepata mabao 409. 

Kwa sababu ulichezwa kwa mfumo wa watu 7 dhidi ya 7, mchezo huo haukuchukuliwa rasmi kama mchezo wa kandanda na hivyo rekodi hiyo itatambuliwa na warusi wenyewe. 

Kwa muda huo wa masaa 26, wachezaji walitakiwa kucheza kwa masaa mawili mfululizo, na kisha kuchukua mapumziko ya dakika nane za kuoga.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet