JE, WAJUA: Mke atumia Helikopta kumtorosha mume wake Gerezani
Eric Buyanza
April 15, 2024
Share :
Mwaka 1986, mwanamke mmoja wa kifaransa alisoma kwa miezi kadhaa jinsi ya kurusha helikopta.
Kwa kutumia ujuzi wake alioupata, alikodi helikopta nyeupe na kuruka nayo mpaka kwenye paa la gereza alilokuwa amefungwa mumewe jijini Paris na kufanikiwa kumtorosha.
Mume huyo Michel Vaujour alifungwa kwa kosa la wizi wa benki.