JE, WAJUA: Mwaka 2014 tajiri alibomoa nyumba zote kijijini kwao, na kujenga magorofa ili wanakijiji wakae bure
Eric Buyanza
March 4, 2024
Share :
Mwaka 2014 mfanyabiashara na tajiri la kichina, Xiong Shuihuda, alibomoa nyumba zote za udongo kwenye kijiji alichozaliwa.
Xiong alifanya hivyo kwa makusudi mazuri kabisa, kwani alijenga nyumba za kifahari za ghorofa katika eneo hilo na kuwataka wanakijiji wote kuhamia humo na kukaa bure bila kulipa kodi yoyote.