JE WAJUA: Radi ilipiga uwanjani na kuua wachezaji 11 wa timu moja tu!
Eric Buyanza
March 28, 2024
Share :
Huko kwenye jimbo la Kasai nchini Kongo mnamo Oktoba mwaka 1998 lilitokea tukio la ajabu kwenye mchezo wa kandanda.
Wachezaji 11 wa timu ya mpira wa miguu ya Bena Tshadi walikufa wote kutokana na radi kali iliyopiga uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya timu ya Basangana.
Cha kushangaza hakuna mchezaji hata mmoja wa Basangana aliyeguswa na radi hiyo.
Wakongo wengi walilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.