JE, WAJUA: Rais huyu alihukumiwa kifo akakimbilia nchini Zimbabwe
Eric Buyanza
June 4, 2024
Share :
May 27 mwaka 2008 mahakama ya juu nchini Ethiopia ilimhukumu kifo Rais wa zamani wa nchi hiyo Mengistu Haile Mariam baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya maelfu ya watu wakati wa utawala wake.
Hata hivyo Mengistu alikimbilia nchini Zimbabwe ambapo amepewa hifadhi baada ya utawala wake kupinduliwa mwaka 1991.
Kwasasa Rais huyo wa zamani wa Ethiopia ana umri wa miaka 83 na anaishi kwenye jiji la Harare.