JE, WAJUA: Robert Pershing, ndiye binadamu mrefu kuwahi kutokea
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Robert Pershing Wadlow, aliyejulikana kwa jina la utani kama 'Jitu la Illinois', alikuwa mwanaume wa kimarekani aliyeingia kwenye rekodi ambayo haijavunjwa mpaka leo ya kuwa mtu mrefu zaidi kuwahi kutokea duniani.
Robert alizaliwa Februari 22, mwaka 1918 na kukulia huko Alton, Illinois, mji mdogo karibu na St. Louis, Missouri.
Alikuwa na urefu wa futi 9 kasoro, yaani futi nane na inch kumi na moja (8.11 in).
Alifariki akiwa amelala Julai 15 mwaka 1940 akiwa na miaka 22.