JE WAJUA: Sark Prison ndilo Gereza dogo kuliko yote duniani
Eric Buyanza
May 30, 2024
Share :
Kisiwa cha Sark, ambacho ni kidogo zaidi kati ya Visiwa vya Channel vilivyo kati ya Ufaransa na Uingereza, ni maskani ya Gereza dogo zaidi duniani (Sark Prison) ambalo bado linatumika.
Hakuna magari, hakuna barabara wala hakuna taa za barabarani kwenye Kisiwa hicho, lakini kuna gereza dogo lililoanza kutumika mwaka 1856 lenye uwezo wa kuhifadhi wafungwa wawili tu.
Licha ya udogo wa gereza hilo, lakini iliwachukua wenyeji wa eneo hilo miaka 20 kulijenga kutokana na ukata wa fedha.
Kisiwa hicho kwasasa kina wakazi 562.