pmbet

Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi aliyeahidi kumuoa

Eric Buyanza

March 22, 2024
Share :

Mahakama ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkulima Stanford Theobert (19) mkazi wa Maporomoko, Tunduma, kwa kosa la kumbaka mwanafunzi baada ya kumdanganya mwanafunzi kuwa atamuoa.
 

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Januari 23, 2023 maeneo ya Kata ya Maporomoko Mjini Tunduma ambapo alituhumiwa kumdanganya kuwa atamuoa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 na kumbaka jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 130 (2) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 ya mwaka 2022.
 

Akisoma maelezo ya hukumu ya kesi hiyo yenye kesi namba 23/2023 Hakimu mkazi wa Wilaya ya Momba Timothy Lyon alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa la kubaka na kumhukumu adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet