pmbet

Jela miaka 30 kwa kumbaka shangazi yake

Eric Buyanza

October 15, 2026
Share :

Mahakama ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu Reiga Innocent (21), mchimbaji wa madini na mkazi wa Iwindi, Mamlaka ya Mji Mbalizi , kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka shangazi yake mwenye umri wa miaka 63.

 

Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba 13, 2026 na Hakimu wa mahakama hiyo, Tedy Mrimba, baada ya mahakama kuridhika kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 29, mwaka huu.

 

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya tukio, mshtakiwa alifika nyumbani kwa mhanga majira ya jioni na kumkuta akiwa peke yake, kabla ya kumshika kwa nguvu na kumbaka.

 

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Imelda Luko, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo, kwa lengo la kukomesha vitendo vya ukatili wa kingono.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet