Jemedari afafanua kuwa Jeraha la Munula
Sisti Herman
March 28, 2024
Share :
Mchambuzi wa michezo ambayer pia ni meneja wa wachezaji Jemedari Said amefafanua kuhusu jeraha la kipa wa klabu ya Simba Aishi Manula alilopata kwenye mchezo wa kimataifa kati ya Tanzania na Bulgaria.
Aishi hawezi kucheza leo, kesho wala wiki ijayo, amepata tatizo sawa na lile alilopata mwanzo lilimfanya afanyiwe upasuaji, nimekuja naye anatembea anavuta mguu" alisema Jemedari kupitia EFM Radio.
Manula ameumia kipindi Simba inajiandaa na michezo ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa Afrika ambapo kwenye robo fainali watacheza kesho dhidi ya Al Ahly.