Jenerali wa Urusi ajeruhiwa kwenye shambulio la Ukraine
Eric Buyanza
August 19, 2025
Share :
Jenerali Esedulla Abachev, naibu kamanda wa vikosi vya Kaskazini mwa Urusi, amejeruhiwa vibaya akiwa mstari wa mbele wa vita na Ukraine, afisa mkuu alisema Jumatatu.
Taarifa za kijasusi kutoka Ukraine zimesema Abachev alikatika mkono na mguu baada ya kujeruhiwa katika shambulio la Ukraine katika eneo la Kursk magharibi mwa Urusi, na kwamba alikuwa akitibiwa mjini Moscow.
Takriban majenerali 12 Urusi wameuawa katika vita vilivyoanza na uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine Februari mwaka 2022.
BBC